Breaking

Wednesday, March 5, 2025

"Baada ya kuwa rais, nilimwambia mlinzi wangu twende kwenye mgahawa kwa ajili ya chakula cha mchana. Tuliketi chini, kila mmoja wetu akaagiza alichotaka.Katika meza ya mbele, kulikuwa na mtu aliyekuwa akisubiri kuhudumiwa. Alipohudumiwa, nilimwambia mmoja wa askari wangu: nenda ukamwambie huyo bwana aje ajiunge nasi. Askari alienda na kumfikishia mwaliko wangu. Yule bwana alisimama, akachukua sahani yake na kuketi karibu nami.Alipokuwa anakula, mikono yake ilitetemeka bila kukoma, na hakunyanyua kichwa chake kutoka kwenye chakula. Tulipomaliza, aliaga bila kuniangalia, nikamshika mkono na akaondoka.Askari alinambia:"Madiba, huyo mtu lazima alikuwa mgonjwa sana, maana mikono yake haikuacha kutetemeka alipokuwa anakula.""Nikajibu: Hapana, sababu ya kutetemeka kwake ni nyingine."Kisha nikamweleza:"Huyo mtu alikuwa mlinzi wa gereza nilikokuwa nimefungwa. Baada ya kunitesa, nililia na kupiga kelele nikiomba maji, lakini badala ya kunipa maji, alinikashifu, akacheka, na akanidhalilisha kwa kunimwagia mkojo kichwani.Hana ugonjwa wowote, bali alikuwa na hofu kuwa mimi, sasa rais wa Afrika Kusini, ningemtupa gerezani na kumfanyia kile alichonifanyia. Lakini mimi si mtu wa aina hiyo; mwenendo huu si sehemu ya tabia yangu, wala maadili yangu.‘Akili zinazotafuta kisasi huharibu mataifa, wakati zile zinazotafuta maridhiano hujenga mataifa.’ Nilipotoka mlangoni kuelekea uhuru wangu, nilijua kwamba kama nisingeacha hasira, chuki, na kinyongo nyuma yangu, ningebaki kuwa mfungwa."Kama kuna chochote umejifunza hapa bonyeza share🙏🏽

No comments:

Post a Comment